Kutoa ruzuku

Ruzuku zinazozingatia matokeo zina lengo la kurahisisha uwezeshaji kisheria pamoja na kuongeza juhudi za kulinda haki za wanawake kuhusu ardhi, mali, usalama na ulinzi. Utoaji wa ruzuku unasaidia wabia wetu kupanuka na kuendeleza upatikanaji wa huduma za msaada wa Kisheria. Kwa kuongezea, ruzuku zinatoa fursa kwa kuimarisha mashirika au taasisi zinazopokea ruzuku, jambo linalochangia kufanya msaada wa Kisheria kuwa endelevu.Uwezo wa maendeleo

LSF inasaidia watoa msaada wa Kisheria kitaasisi na kiufundi, jambo ambalo linasaidia katika uhamasishaji wa rasilimali. Mchango zaidi ni kuongeza uwajibikaji, uwazi na ubora wa utoaji wa msaada wa Kisheria. Hii itakuwa na matokeo chanya kukubali huduma za kitaasisi kwa wale wenye wajibu ili kusaidia kuweka mazingira mazuri kwa uwezeshaji kisheria.Ubia, kuwa na mtandao na kutafuta fedha

Hii inalenga kuthibitisha na kurahisisha mchango wa LSF kwa kuanzisha rasilimali fedha na kufanya vituo vya utaalam ili viweze kufikika kwa urahisi. Hii ni pamoja na kusaidia mitandao ya msaada wa Kisheria na ushirikiano katika kulinda haki za binadamu.Uratibu

LSF iko makini katika kuratibu shughuli za upataikanji haki kwa wote, hasa wanawake. Utoaji wa msaada wa Kisheria ya uwezeshaji kisheria mijini na Zanzibar ni mifano miwili.Kujifunza

Kujifunza kunakuzwa kwa kuweka bayana ni kitu gani kinafanya kazi na kitu gani hakifanyi kazi.Tunajaribu njia mbalimbali na tunawafuatilia wabia wetu kwa umakini, jambo ambalo linatoa mwelekeo wa mpango wetu. Kuhakikisha uwajibikaji kwa umma na kuchangia msingi wa uelewa wa msaada wa Kisheria, elimu na uwezeshaji kuhusiana na upatikanaji wa haki na kwa mawasiliano ya kitaaluma vinaendelezwa.