Nani anaweza kuomba ruzuku?

Mfuko wa LSF unatoa ufadhiri kwa mashirika yenye nia thabiti ya kuongeza upatikanaji wa haki sawa kwa wote, hasa kwa wanawake na wasichana. Hili linaweza kufanyika kwa kuboresha kiwango cha utoaji huduma za misaada ya kisheria na kuongeza upatikanaji wake. Hivyo mashirika yanayoshughulika na kuongeza uelewa wa masuala ya haki za binadamu, elimu ya sheria, kujitambua kuhusu sheria, na kupigania na kulinda haki za wanawake yanaweza kutuma maombi yao wakati wowote tunapokuwa tumetangaza kukaribisha maombi. Pia LSF inapenda kupanua wigo wake kwa kushirikiana na mashirika yanayolenga kujipambanua katika kuwajengea wananchi uwezo wao kiuchumi na kisiasa kwa kutumia kipengele cha uwezeshaji wa kisheria.


Ili kukidhi kigezo cha kuomba ruzuku kutoka LSF, lazima liwe shirika lililosajiliwa na lisilokuwa na kiserikali wala kuendeshwa kwa lengo la kutengeneza faida ya kifedha.


Namna ya kuomba ruzuku?

LSF huwa inatoa tangazo kukaribisha maombi au pendekezo la ruzuku kutoka kwa mashirika mbalimbali nchini. Tangazo hilo linatolewa katika magazeti makubwa ya Kiswahili na Kingereza, kwenye tovuti hii, na pia katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii kama vile facebook na twitter. Pamoja ta tangazo hili, huwa maudhui yanayotakiwa kwenye maombi, miongozo ya uwasilishi wa maombi na fomu za maombi hupatikana katika tovuti hii na pia katika ofisi zetu (angalia anauni yetu).Nini kinafadhiliwa na mfuko?

LSF utoa fedha kwa mashirika watekelezaji katika ngazi ya mkoa ambapo wao sasa uratibu na kutekeleza mpango wa uwezeshaji ama uanzishwaji wa vituo vya kisheria (Paralegal Units) katika wilaya zote zinazounda mkoa husika.


Pia, LSF inaweza kutoa ruzuku kwa ajili ya masuala ya kujenga uelewa wa haki za binadamu, elimu ya sheria, uwezeshaji wa kisheria, na mengine yote yanayohusu uwezeshaji wa kijamii, kiuchumi, na kisiasa nchini Tanzania.