LSF ni mfuko huru wa msaada wa kisheria uliosajiliwa mwaka 2013 kama shirika lisilo la kiserikali na lisilofanya biashara na kupata faida lenye makao makuu yake Dar es Salaam. LSF ni shirika linalojitahidi kuongeza fursa za upatikanaji wa haki kwa wote, hasa wanawake kwa njia ya uwezeshaji. Tunatoa msaada wa kifedha kwa kuzingatia usawa kwa mashirika yanayounga mkono, kutoka ama kusaidia kutoa misaada wa kisheria, huduma za wasaidizi wa kisheria na yanayofanya kazi kuwawezesha wanawake maskini, watoto na wanaume.
Kupitia huduma hizi, watu binafsi na jamii kwa ujumla wanasaidiwa kuhakikisha haki zao zinalindwa, malalamiko yao yanashughulikiwa, migogoro yao inatatuliwa na haki zao za msingi za binadamu zinalindwa na kupiganiwa. LSF wanafadhili shughuli za uwezeshaji wa kisheria katika wilaya zote 180 za Tanzania Bara na Zanzibar. Tunafanya kazi pamoja na kuishawishi serikali ili itimize wajibu wake wa kutunga sheria inayowezesha utoaji wa msaada wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuwatambua wasaidizi wa kisheria, ambao bado wanahitaji kutambuliwa na kufadhiliwa.
Tunasaidia moja kwa moja na kupitia njia nyingine zaidi ya mashirika wabia 200, ambayo yanahakikisha kunakuwepo na huduma sawa na rahisi za msaada wa sheria, elimu ya sheria na kurahisisha uwezeshajikisheria kwenye jamii wanaitumikia.
Jamii ya Kitanzania ambamo watu wote wana fursa ya kupata haki.
Kukuza na kulinda haki za binadamu kwa njia ya uwezeshaji kisheria, kuongeza upatikanaji wa huduma za sheria kwa wanajamii maskini na walio kwenye mazingira magumu, hasa wanawake.
Kuongeza upatikanaji wa haki kwa wote, hasa wanawake.
LSF inaona malengo maalum kama masharti ya awali kwa kufikia lengo la kuongeza fursa za upatikanaji wa haki: